Tuesday, August 30, 2016

Mbinu za kuacha uvutaji wa sigara


Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu kuachana na uvutaji wa sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara yake, lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana katika tumbaku.

Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kufuata mkumbo, lakini baadaye wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo.

Hata hivyo idadi kubwa ya wanaojaribu kuacha wamejikuta wakipata majibu ya kutoweza, kutokana na kusumbuliwa na hamu ya uvutaji, umbumbu wa mawazo pindi wanapokaa muda mrefu bila kuvuta, kuumwa na kichwa na hata udhaifu katika kukumbuka vitu au mambo waliyofanya au waliyopanga kuyatenda.

Pamoja na yote hayo watalaam na washauri wa masuala uvuaji wa sigara wanasema wanaopatwa na hayo wamekosa mbinu na muongozo wa kuwasaidia waachane na uvutaji wa sigara bila kupata madhara.

Kwa ufupi somo hili limehusisha uchunguzi wa kina pamoja na kumbukumbu za kitaalamu kutoka kwa washauri kama Anderson JE, Jorenby DE, Scott WJ, Fiore MC, Bailey WC, Cohen SJ, ambao wote kwa pamoja kupitia vituo vyao kikiwemo cha US Department of Health and Human Services na Public Health Service walishawahiwa kueleza mbinu salama za kuachana na uvuaji wa sigara. Zifuatazo ni dondoo kadhaa za kufuata ili mvutaji aache sigara kwa usalama.

* Mvutaji lazima afahamu ni muda gani ambao huwa anavuta sigara kwa wingi, je ni wakati akiwa amelewa au akiwa na mawazo mengi ya kimaisha? Akishafahamu hilo ajiulize ni kiwango gani cha sigara ambacho huwa unavuta kwa siku?

* Baada ya hapo achukua kitabu chake cha kumbukumbu na aandike muda huo ambao yeye huvuta sigara kwa wingi. Ajiulize kwa nini huwa unavuta, atathimini madhara ya uvutaji wa sigara kwake binafsi na kwa familia yako.

* Kaa chini upitie kwa makini kumbukumbu zako za muda na kiwango cha sigara unazovuta kwa nyakati hizo, kisha panga utaratibu mpya. Kwa mfano kama unavuta sana wakati ukiwa kwenye mawazo hakikisha kuwa unapoanza kufikiria juu ya jambo fulani uwe na kitu mbadala kitachukua nafasi ya sigara. Mfano kahawa au chai? Hakikisha kila penye hamu ya uvutaji unaweka kitu kingine mbadala cha kufanya zaidi ya kuvuta sigara.

*Ondoa masalio ya sigara katika sehemu ambazo unaishi, fua nguo zote na vitambaa ili kuondoa harufu ya sigara katika eneo unalokuwepo. Usikae karibu na mtu anayevuta, usikubali kuwa mshirika wa mvutaji na usiwe mtu wa kuendekeza sana msukumo wa mwili unaotaka uvute, bali kila unapowaza juu ya kuvuta fikiria madhara na nia yako ya kuacha.

*Wafahamishe rafiki zako kuwa umeamua kuachana na uvutaji, ili upate watu wa kuwaonea aibu pale utakapoanguka na kurudia uvutaji wa sigara. Panga tarehe ya kuacha na iwe kwenye kumbukumbu.

*Wakati ukiiendea tarehe hiyo ya kuacha hakikisha unapunguza kiwango cha uvutaji kadiri unavyoisogea siku hiyo. Jipangie muda mrefu zaidi ya kuvuta kulingana na kiwango chako cha uvutaji na kuendelea kuuongeza kila siku ili uzoee kukaa saa nyingi bila kuvuta.

*Fuata ratiba mbadala uliyojiwekea kuziba pengo la uvutaji, kama umepanga kutumia kahawa kila unapokuwa mpweke sebuleni hakikisha unajizoeza ili ikifika tarehe yako ya kuacha usiwe mtu wa kujiuliza cha kufanya nyakati ambazo utakuwa na hamu ya sigara.

*Lengo lako liwe ni kufanikiwa na usikate tamaa utakaposhindwa kufanikisha lengo lako kwa wakati uliojipangia. Mara kwa mara nenda kamuone daktari mshauri ili akupe muongozo zaidi wa kukusaidia na ikiwezekana akupe nafasi ya kuwatembelea wagonjwa waliopata ugonjwa wa kifua kwa sababu ya kuvuta sigara.

Kwa kifupi hizo ni dondoo chache tu za kukusaidia kuachana na uvutaji wa sigara, lakini mara nyingi kinachoweka nguvu za kufanikisha uachaji wa sigara ni utashi wa mtu ambao hutokana na tathimin ya kina ya muhusika na mtazamo wake juu ya sababu za kuacha. Mara nyingi wanaoshindwa ni wale ambao hawakuzitia nguvu sababu za kuacha kwao.

Siku zote mwanadamu anaongozwa na utashi na kila mwenye kutaka hufanikiwa. Hii ina maana kuwa kama mwanadamu atasema hawezi kuacha kitu fulani, haina maana kama hawezi kwa sababu ameshindwa kujizuia bali ameamua kutokutaka na kinachomshinda ni matokeo ya  maamuzi yake. Kila anayetaka jambo hufanikiwa na hata wavutao sigara wanaweza kuacha kama wakitaka kufanya hivyo.

KUUMWA TUMBO WAKATI WA HEDHI


KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya.Kutokana na simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata akina mama wengi wakati wa hedhi nimeona ni bora niandike makala hii ili iweze kuwasaidia na wengine kujua nini chanzo na mhusika afanye nini pale anapopatwa na tatizo hilo.

Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.

Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu hayo huanza pale yai linapotoka katika mrija (fallopian tube) na kuteremka chini ya mrija huo wakati wa Ovulation.

AINA YA MAUMIVU
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.
  • Ya kwanza  ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. 
  • Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. 
  • Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.


Aina ya pili  ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.

Nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia kumi mpaka kumi na tano  wanasema kuwa hupata maumivu makali.

Uchunguzi unaonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.

Sababu hizo ni kama  kuwa na umri wa chini ya miaka 20, kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo, kutoka  damu nyingi wakati wa hedhi, wanawake ambao hawajawahi kuzaa.

Magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:

Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo.

Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaota katika mfuko wa uzazi.

PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.

  1. Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
  2. Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.
  3. baadhi ya magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. niliishia kuelezea ugonjwa wa uvimbe katika nyonga ambao husababishwa na magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya zinaa.


Dalili za ugonjwa huo ni:

  • Maumivu kuja na kuondoka, kwa kiwango tofauti (spasmodic).
  • Maumivu zaidi huwa sehemu ya chini ya tumbo na huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo ambayo husambaa mpaka mapajani.
  • Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.
  • Kupata choo laini au hata kuharisha na wengine hufunga choo.


TUMBO KUWA KUBWA AU KUWA GUMU.

  • Kupata maumivu ya kichwa, kujisikia kuchoka.
  • Kiwango cha maumivu ya tumbo la hedhi na mchanganyiko wa dalili inategemea mtu na mtu, mtu mwingine anaweza akawa anapata karibu dalili zote nilizozitaja hapo juu na mwingine ni baadhi tu au hata dalili moja. Wanawake wengi hujitambua  bila hata msaada wa daktari.


USHAURI
Iwapo mwanamke atapata maumivu makali sana ni bora akamuone daktari ili wafanye vipimo kama vile Ultrasound, CT na CT-Scan, MRI na vinginevyo ili kufahamu nini chanzo cha  maumivu hayo kuwa makali.

MATIBABU
Matibabu ya maumivu ya tumbo la hedhi kwa kawaida huweza kutibika kwa urahisi kwa kutumia vidonge vya kupunguza maumivu, kama vile Ibuprofen, naproxen au aina nyinginezo za vidonge visivyokuwa na steroids (NSAIDS). Pia kuna wakati madaktari wanaweza kumshauri mgonjwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba, Vidonge hivyo huzuia mzunguko wa yai au Ovulation na kupunguza ukali wa maumivu ya tumbo la hedhi.

Pia  wanawake wanashauriwa kufanya baadhi ya vitendo ambavyo hupunguza maumivu  hayo, kama kuoga maji moto, kuweka kitambaa chenye joto katika sehemu ya chini ya tumbo, kufanya mazoezi kama yoga, meditation,  kutumia vidonge vya vitamin E, Thiamine na Omega 3 kumetajwa kuwa husaidia katika suala hilo. Wanawake wanaopatwa na matatizo kama

hayo ni bora wapumzike vyema na kupata usingizi wa kutosha.
Vilevile unaweza kujiepusha na kupatwa na maumivu ya tumbo la mwezi kwa kufanya yafuatayo:
Kujitahidi kula matunda, mbogamboga na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi, pombe, kafeini, sodium na sukari, kufanya mazoezi ya viungo, kujiepusha na wasiwasi na mawazo na kuepuka kuvuta sigara.

Jinsi mgonjwa wa kisukari anavyoweza kuepuka kiharusi (kupooza) au stroke


Ni dhahiri kuwa wagonjwa wengi siku hizi wamekuwa wakikumbwa na tatizo hili la kupooza ambalo wengi huwakumba ghafla wakiwa hawana ufahamu wowote nini ambacho kimetokea.

KUPOOZA
Hii ni ile hali ya kiungo kupoteza utendaji kazi wake kwa sababu ya neva za fahamu kuathiriwa.

2.       KIHARUSI AU STROKE
Hii ni ile hali ya ubongo kupata hitilafu katika kupokea damu na hatimaye kupelekea kupooza kwa viungo baadhi au mwili mzima. Na endapo seli za ubongo zikikosa damu na oksijeni kwa dakika 3 zinaanza kufa na kupoteza utendaji kazi wake na endapo hili tatizo lispo shughurikiwa ndani ya masaa matatu dalili zake zinakuwa zimefikia pabaya sana katika matibabu.

Sasa basi ningependa kuongelea kidogo kuhusu ugonjwa huu na jinsi gani unaweza kujizuia.


SABABU ZISIZO EPUKIKA
Napenda kusema kwamba, Katika kitabu cha The China Study kilicho andikwa na Prof. Collin Campbell kinasema kwamba, kila binadamu ana chembe chembe za vina saba yani DNA za urithi kutoka kwa wazazi wetu ambazo zinarithishwa kila kizazi. Hivyo kila mtu ana viini vya urithi vya magonjwa mbalimbali kutoka kwa wazazi wetu, ni jukumu lako kufanya chembe chembe hizo zijioneshe wazi wazi. Hivyo bwana Campbell ambaye ni mtafiti mashuhuri wa lishe na magonjwa alisema kuwa, ni jukumu lako wewe kuuchokoza mwili wako uwezo kuonesha magonjwa ambayo umeyarithi kutoka katika ukoo wenu. Endapo ukiishi maisha ya kiafya, kula vizuri vyakula vya asili hutasumbuka na magonjwa tabia kama kisukari,shinikizo la damu,uvimbe kwenye kizazi,ugumba,kansa nk.

Kwa sababu tumeshindwa kuishi maisha ya uhalisia wetu,tunaishi kwa kufurahia vyakula vilivyofanyiwa marekebisho na binadamu na kufurahia bei yake ilivyo ndogo katika kiwango cha kujitosheleza, Basi swali la kujiuliza ni kwa nini vyakula hivyo vya viwandani vinauzwa bei ya chini sana kuzidi vyakula asili? Hebu nenda leo ukanunue nyanya ambazo unaweza kukamua ukapata chupa moja ya 400mls! UTAGHARIMIKA PESA KUBWA KULIKO YULE ALIYENUNUA Nyanya iliyotengenezwa kiwandani na kuwekwa kwenye chupa maalumu, Jiulize tena Kwa nini vinauzwa bei ya kiwango cha chini kiasi hicho?

Mwenendo huo wa maisha ya ulaji vyakula vya viwandani,vinywaji vyenye sukari nyingi,radha,rang ink, unatufanya tuwe na vihatarishi vya kupata ugonjwa wa kupoooza bila kuwa na uwezo wa kuepuka hadi pale tutakapo badili mwenendo wa maisha yetu.



1.       UMRI
Tafiti zinaonesha kuwa kadri umri wako unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo unavyozidi kuwa hatarini sana kukumbwa na tatizo la kupooza. Umri Zaidi ya miaka 50 upo katika hatari kubwa sana ya kupata magonjwa yatakayokupelekea kupata kiharusi. Kwani kiharusi ni ugonjwa moja wapo utakao kupelekea kupooza kwa baadhi ya viungo vya mwili wako na haimaye mwili mzima.
Hivyo kama wewe bado hujafikia katika umri huu, basi ni wakati wa kuishi katika lishe asili  Inatoka katika mashamba yetu ya wakulima.


2.       JINSIA
Tafito zinaonesha kwamba wanaume wako hatarini sana kupata kiharusi ukilinganisha na jinsia ya kike. Lakini pia tafiti zinaonesha kuwa kati ya mwanamke na mwanaume, mwanamke ndiye yupo hatarini sana kupata kifo kitokanacho na kiharusi. Hivyo endapo mwanamke akipatwa na kiharusi maendeleo yake kuanzia anapopatwa na tatizo huwa sio mazuri sana ukilinganisha na mwanaume. Hivyo mwanamke huwahi kukutwa na kifo Zaidi ukilinganisha na mwanaume anaweza kukaa muda mrefu sana.

3.       URITHI
Kuna watu wenye historia kuwa katika ukoo wao kuna watu wenye matatizo ya kiharusi au babu, bibi alikumbwa na tatizo hilo. Hivyo hata wewe unaweza ukawa hatarini kupata tatizo kama hilo endapo tu maisha unayo ishi nayo yakiwa ni maisha yasiyo jumuisha lishe ya asili ninayopenda kuita lishe ya dawa.

4.       KAMA UMESHAWAHI KUPATWA KIHARUSI KIDOGO
Hii ni aina ya kiharusi inayotokea kwa muda mfupi na kupotea. Muda mwingine huwa ni vigumu kutofautisha na kiharusi chenyewe. Maana kiharusi kidogo (Transient Ischemic Attach) husababisha pia viungo kupoteza utendaji kazi wake na inaweza pia kuathiri utendaji kazi wa ubongo kiakiri pia. Hivyo kama umeshaga wahi patwa na TIA kipindi cha nyuma, uwezekano wa kupata tena ni mkubwa sana, na unaweza kupata kiharusi kabisa chenyewe.


Hapo juu nimesema kuwa ni vihatarishi visivyozuilika LAKINI ni kwa wale wasioweza kubadili mienendo ya maisha ya kifahari na kujiepusha na magonjwa tabia kama kisukari,shinikizo la damu na kiwango kikubwa cha lehemu mwilini mwako


SABABU UNAZOWEZO KUZISABABISHA WEWE MWENYEWE NA KUKUPELEKEA KUPATA KIHARUSI ( STROKE)

1.       MAGONJWA YA MOYO
Magonjwa ya moyo kwa umri Zaidi ya miaka 60 imekuwa ni kawaida kutokana na miili yetu kuwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini mwetu na miili yetu kuwepo katika mazingira ya kupokea vyakula visivyo vya msingi katika kuboresha utendaji kazi wa mwili wako na tofauti na kuharibu uwezo wa mwili wako kufanya kazi ipasavyo.

Moja wapo ya magonjwa yanayopelekea kupata kiharusi, ni pale moyo wako unaposhindwa kutengeneza umeme wa kutosha kutoka juu kwenye vyumba vya moyo viitwavyo Atria na hatimaye kusambaa kwenye vyumba vya chini vya moyo viitwavyo Ventriko. Hivyo basi napenda kukuambia kuwa, moyo hutengeneza umeme, na umeme huo huzunguka kwenye sakiti ya umeme wa moyo, sakiti hio huanzia kwenye vyumba vya juu vya moyo na kushuka vyumba vya chini na hatimaye kusambaa katika misuli yote ya moyo na hatimaye kusukuma damu kutoka kwenye moyo. Hivyo kunapokuwa kuna hitirafu katika utengenezwaji wa umeme kuanzia sehemu husika, umeme unatengenezwa usiotosheleza na unatoka sehemu mbalimbali (sio maalumu) unajikuta misuli ya moyo inapata umeme kutoka katika vyanzo tofauti na umeme huo hautoshelezi kuweza kusukuma damu ipasavyo. Ugonjwa huu kwa lugha ya kiratini tunaita Atrial Fibrillation. Hivyo moyo wako unapokuwa na tatizo hili, hata mapigo ya moyo hubadirika. Njia pekee ambayo unaweza ukajigundua kuwa una tatizo hili, ni kuangalia kiashiria cha mapigo ya moyo sehemu mbali mbali kama shingoni,juu ya mkoni wako karibu na kiganja kama mapigo ya moyo yanaenda sawa au laa! Pia unaweza kwenda Zaidi kufanya uchunguzi kama kipimo cha ELECTROCARDIOGRAM (ECG) unaweza kupata majibu halisi kuwa umeme huo unajitosheleza au laa! Na unatengenezwa kutoka katika chanzo kimoja au laa! Pia moja ya sababu moja wapo ni kuangalia misuli ya moyo na kiwango cha damu kinachosukumwa na myo wako, ni vyema pia ukipata kipimo kingine cha moyo kinaitwa ECHOCARDIOGRAM(ECHO) hiki kinakupa taarifa zote za kiwango cha damu kinachosukumwa,ukubwa wa misuli ya moyo, na taarifa zinginezo. Kumbuka vipimo hivi vinapatikana katika hospitali kubwa za rufaa na vinategemea umahili wa mpimaji na msomaji wa majibu yako.

Ugonjwa huu wa moyo unaweza kusababisha kiharusi kwa sababu moja kuu kwamba, pale moyo unaposhindwa kutenegeneza umeme wa kutosha kusukuma damu, kutakuwa na mrundikano wa tamu kwenye moyo na damu hio inaweza kuganda na hatimaye kusukumwa kwenda kwenye mishipa midogo ya ubongo na kusababisha kizuizi cha damu kufika kwenye ubongo kwa sababu ya kutwama kwa damu iliyo ganda. Hivyo ndivyo unaweza kupata kiharusi endapo moyo wako hautengenezi vizuri umeme wake.





2.       KIWANGO KINGI CHA CHOLESTERO(LEHEMU) MBAYA MWILINI MWAKO

Lehemu kwa tafsiri nyepesi ni fati(mafuta) ambayo ipo kama nta ( wax) huzunguka sehmu mbalimbali katika mwili wako kwa kupitia mfumo wa mzunguko wa damu.
Ikumbukwe Lehemu ina kazi kubwa sana miilini mwetu kama kutengeneza seli za mwili na kutengeneza homoni za miili yetu na kazi zingine nyingi. Hivyo basi ningependa kukuambia kuwa kuna ina kuu tatu za lehemu ambazo ningependa kuzitaja kwa ufupi katika makundi makuu mawili, Lehemu mbaya ambayo inajulikana kama Low density Lipoprotein (LDL)  pia na Triglycerides na aina ya pili ni lehemu nzuri ijuilikanayo kama Hingh density Lipoprotein –HDL.

Lehemu inaweza kusababisha kiharusi kwa sababu ya tabia yake mbaya ya kunasa kiurahisi kwenye kuta za mishipa ya ateri na hatimaye kupunguza kipenyo cha mshipa wa damu au kuziba kabisa na hatimaye kuzuia damu kufika vizuri katika ubongo na hatimaye ubongo hukosa damu na oxygen.

Tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa nyama za aina yoyote ile, zina kiwango kingi sana cha lehemu mbaya ambayo inaenda kutuathiri sana. Lakini pia tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa vyakula vya mboga za majani, matunda vinasaidia sana kuepukana na lehemu mbaya na kumaliza kabisa matatizo yanayo sababishwa na lehemu mbaya mwilini mwako.
Rehemu hujulikana kama kisababishi kikubwa cha aina moja wapo ya kiharusi kinachosababishwa na mishipa midogo ya damu kutopitisha damu na kuulisha ubongo wako vizuri na hatimaye seli za ubongo huanza kufa nah ii hutokea baada tu ya ubongo kukosa damu kwa muda wa dakika tatu.

Aina hii ya kiharusi huitwa ISCHEMIC STROKE (Ischemia, Ni ile hali cha seli za mwili kufa Kwa kukosa oxygen, na Stroke ni kupooza). Hivyo Ischemic stroke ni kupooza kunako sababishwa na kukosa hewa ya oksijeni kwenye ubongo kwa sababu ya kukosa damu kwenye ubongo kunakosababishwa na kuziba kwa mishipa midogo midogo inayopeleka damu kwenye ubongo.

Unaweza kuchunguza kiwango chako cha lehemu kama kingi au laa! Unaweza kwa kuchunguza kitalamu kwa kuchukua sampuli ya damu na kupeleka maabala (Biochemistry Lab) na hatimaye utapata majibu yako. Pia unaweza ukatumia vipimo vingine vya picha vinavyopima kiwango cha lehemu mbaya moja kwa moja kwenye mishipa ya damu Angiogram na pia unaweza kupima kwa kutumia Kipimo cha kuangalia uzalishaji wa umeme kwenye moyo kwani lehemu ni chanzo kikubwa sana cha kuharibu utendaji kazi wa moyo hivyo kipimo cha Electrocardiogram kinaweza pia kutumika na kuangalia moja kwa moja.



Note: Napenda kutoa angalizo kuwa vipimo vingi ninavyotaja hapo ni vikubwa sana na gharama yake kidogo kubwa na vingi vinapatikana hospitali ya rufaa na kwenye vituo mbali mbali binafsi. Na hivyo wengi wenu mmekuwa mkiniuliza kama Dr Boaz Mkumbo naweza kuwasaidia kwa hilo. Napenda kuwasaidia kama ninavyokupatia elimu hii ya afya bure kabisa, ushauri wangu ni kwamba vipimo vyote vya kitaalamu vinategemea na mpimaji na msomaji ana taaluma gani katika kusoma majibu.

Kama mpimaji akipotosha na daktari anayetibu atapotoka na hapa ndipo madhaifu makubwa ya vipimo hivi vingi na ndio maana magonjwa mengi tunashindwa kuyabaini mapema kwa kukosekana kwa ufanisi kwa watu wanaopima. Sasa ningependa kukupa siri moja ya vipimo vyote nilivyo vitaja hapo juu, Vina hitaji umahili mkubwa wa kusoma majibu, na vituo vingi binafsi havina watu mahili wa kusoma vipimo hivi ,viko pale kama kitega uchumi kukushusha roho kuwa umepima. Tatizo sio kupima, Kiu ni kugundua ugonjwa sahihi na utibiwe upone. Ningependa kukushauiri kama unahitaji vipimo hivi, fika hospitali yenye wataalamu wa kutosha wenye uwezo mkubwa wa kukupa majibu ya uhakika ya kukata kiu yako.

- American Diabetes Association Inashauri kiwango cha LDL cholesterol kuwa chini ya 100 mg/dl kwa watu wenye kisukari na chini ya 70 mg/dl kwa watu wenye magonjwa ya moyo.
-Pia inashauri kuwa kiwango cha lehemu nzuri yani HDL iwe 50 mg/dl au Zaidi kwa wanawake na kwa wanaume HDL iwe 40 mg/dl au Zaidi.


3.       SHINIKIZOLA JUU LA DAMU( HIGH BLOOD PRESSURE)
Shinikizo la damu ni msukumo wa damu ndani ya mishipa ya damu thidi ya ukuta wa mishipa. Shinikizo la damu lenye takwimu ya Zaidi 140/90 mmhg kwa muda mrefu utakuwa unastahili kuitwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu.

Shinikizo kubwa la damu husababisha kiharusi kwa kusababisha mishipa midogo ya damu ya ubongo kupasuka na hatimaye damu kuvia kwenye ubongo. Aina hii ya kiharusi huitwa Hemorrhegic Stroke. Aina hii ya kiharusi ni mara chache sana kutokea na huwa ni nadra sana kukuta mtu ana aina hii ya kiharusi lakini ndio aina nambari moja inayoweza kusababisha kifo haraka sana kwa mgonjwa. Kwani wagonjwa wengi wanaopata aina hii ya kiharusi huwa maendeleo yao sio mazuri na wengi hufika hospitali wakiwa hawajitambui kabisa.

Ugonjwa wa Shinikizo la damu unazuilika kabisa kwa kufuata masharti machache kama haya hapa chini:
Ulaji wa vyakula vya madini ya potasiamu hadi kufikia 3900mg kwa siku kutoka kwenye ndizi,machungwa,matunda yaliyo kaushwa,viazi vitamu nk

Ulaji wa Madini ya Calcium angalau 1200mg kila siku kutoka kwenye vyakula kama mtindi na maziwa ya kuwaida

Ulaji wa vyakula vyenye magnesium angalau 420mg kwa siku kwa wanaume na 320mg kwa wanawake kutoka kwenye vyakula kama Spinachi, nafaka isiyokobolewa, Ndizi nk

4.       KUTOFANYA MAZOEZI YA VIUNGO
Mazoezi siku hizi yamekuwa yakitumiwa na watu pekee wanao hitaji kupunguza mwili na kupunguza nyama uzembe ( belly fats) ,inapendeza sana wadada wengi kuchukia kubadirika kwa miili yao unaotokana na ulaji wa vyakula visivyo asili, Napenda kukuambia kuwa Mazoezi pekee sio SULUHISHO LA KUPUNGUZA MWILI WAKO, NA WALA SIO SULUHISHO LA KUONDOA NYAMA UZEMBE. Bali siku ukijifunza kubadili mwonekano wa sahani yako mezani utafurahia jinsi uzito unavyopungua! Najua huamini, lakini unapokuwa unaanza safari ya kupunguza uzito na nyama uzembe ujue ni safari nzito kama vile safari ya kutafuta pesa. Kupungua uzito sio kurahisi ingekuwa rahisi wengi hawapendi wangekuwa wameshapungua ! Njia pekee ni kujidhatiti na kudhubutu pekee katika kubadili lishe yako, mchawi mkubwa ni sahani yako unayoiweka mbele yako kila utakapo kuweka kitu kinywani mwako.

Mazoezi huimarisha viungo na mzunguko wa damu na kusaidia mwili wako kutoa taka ambazo zimepatikana kutokana na shughuli za mwili.

Tafiti zinaonesha kwamba watu ambao hawafanyi mazoezi ya kutosha katika umri mkubwa huwa hatarini kupata kiharusi aina ya Ishemic stroke inayosababishwa na damu kutosukumwa ipasavyo katika mishipa ya damu na kusababisha  emboli kunasa kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kufika vizuri katika ubongo.


MAKUNDI MENGINEYO AMBAYO SITAPENDA KUYAELEZA KWA KINA LEO
5.       Walevi wa pombe na sigara

6.       Wanaotumia njia za uzazi wa mpango kwa muda mrefu

7.       Watu wenye kisukari kwani kisukari na shinikizo la damu ni bwana harusi na bibi harusi mara nyingi hutembea kwa umoja.


90 DAYS CARDIO FUNCTION-REVERSE PACKAGE
Hii ni program maalumu kwa wasomaji wetu ambao wamekuwa wakisumbuka na magonjwa sugu kama kisukari,shinikizo la juu la damu n ahata shinikizo la chini la damu, kiharusi n ahata tatizo la kupungua kwa utendaji kazi wa ubongo.

Hii program imeandaliwa na Boaz Mkumbo ambapo inawafaa wale wachache wanaohitaji msaada wangu pale walipofikia kutumia elimu hii ya afya ambayo nimekuwa nikiitoa kila siku.

                                  NDANI YA CARDIO FUNCTION REVERSE PACKAGE
1.       Unajipatia msaada wa kupata Suluhisho la kuondoa lehemu zote mbaya mwilini mwako na kuimarisha mzunguko wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili na kuimarisha damu inayoenda kulisha ubongo.

2.       Utajipatia Kiondoa sumu makini kabisa chenye kuzuia mchakato unaendelea mwilini mwako ( Gut and systemic Inflammation) chenye kusheheni madini mengi ambayo ni catalyst ya shughuri nyingi za mwili madini haya husaidia kuupooza mwili kutoka katika mpambano wa maradhi mbali mbali yanayoendelea mwlini mwako, Madini mengi ya Manganeze,zinc,selenium,Iron na mengine mengi kwani kimekuwa ni chakula nambari tatu kama lishe bora duniani

3.       Unaweza kupatiwa ushauri kwa wale waliotayari pata tatizo la kupooza kutokana na kiharusi na presha yako haijakaa sawa, Utapewa huduma nzuri namna gani unaweza pia ukanufaika na mazoezi ya viungo na bidhaa zetu unapokuwa katika matibabu chini ya ushauri wetu.

4.       Napenda kuwaambia kuwa msaada huu ndani ya package hii ya siku 90 tutakusaidia endapo tu , unahitaji kwani wengi wanafurahia huduma zetu za tiba asili na pia ushauri tunatoa kwa watu wenye matatizo ya magonjwa haya sugu.