Friday, September 2, 2016

Tuesday, August 30, 2016

Mbinu za kuacha uvutaji wa sigara


Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu kuachana na uvutaji wa sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara yake, lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana katika tumbaku.

Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kufuata mkumbo, lakini baadaye wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo.

Hata hivyo idadi kubwa ya wanaojaribu kuacha wamejikuta wakipata majibu ya kutoweza, kutokana na kusumbuliwa na hamu ya uvutaji, umbumbu wa mawazo pindi wanapokaa muda mrefu bila kuvuta, kuumwa na kichwa na hata udhaifu katika kukumbuka vitu au mambo waliyofanya au waliyopanga kuyatenda.

Pamoja na yote hayo watalaam na washauri wa masuala uvuaji wa sigara wanasema wanaopatwa na hayo wamekosa mbinu na muongozo wa kuwasaidia waachane na uvutaji wa sigara bila kupata madhara.

Kwa ufupi somo hili limehusisha uchunguzi wa kina pamoja na kumbukumbu za kitaalamu kutoka kwa washauri kama Anderson JE, Jorenby DE, Scott WJ, Fiore MC, Bailey WC, Cohen SJ, ambao wote kwa pamoja kupitia vituo vyao kikiwemo cha US Department of Health and Human Services na Public Health Service walishawahiwa kueleza mbinu salama za kuachana na uvuaji wa sigara. Zifuatazo ni dondoo kadhaa za kufuata ili mvutaji aache sigara kwa usalama.

* Mvutaji lazima afahamu ni muda gani ambao huwa anavuta sigara kwa wingi, je ni wakati akiwa amelewa au akiwa na mawazo mengi ya kimaisha? Akishafahamu hilo ajiulize ni kiwango gani cha sigara ambacho huwa unavuta kwa siku?

* Baada ya hapo achukua kitabu chake cha kumbukumbu na aandike muda huo ambao yeye huvuta sigara kwa wingi. Ajiulize kwa nini huwa unavuta, atathimini madhara ya uvutaji wa sigara kwake binafsi na kwa familia yako.

* Kaa chini upitie kwa makini kumbukumbu zako za muda na kiwango cha sigara unazovuta kwa nyakati hizo, kisha panga utaratibu mpya. Kwa mfano kama unavuta sana wakati ukiwa kwenye mawazo hakikisha kuwa unapoanza kufikiria juu ya jambo fulani uwe na kitu mbadala kitachukua nafasi ya sigara. Mfano kahawa au chai? Hakikisha kila penye hamu ya uvutaji unaweka kitu kingine mbadala cha kufanya zaidi ya kuvuta sigara.

*Ondoa masalio ya sigara katika sehemu ambazo unaishi, fua nguo zote na vitambaa ili kuondoa harufu ya sigara katika eneo unalokuwepo. Usikae karibu na mtu anayevuta, usikubali kuwa mshirika wa mvutaji na usiwe mtu wa kuendekeza sana msukumo wa mwili unaotaka uvute, bali kila unapowaza juu ya kuvuta fikiria madhara na nia yako ya kuacha.

*Wafahamishe rafiki zako kuwa umeamua kuachana na uvutaji, ili upate watu wa kuwaonea aibu pale utakapoanguka na kurudia uvutaji wa sigara. Panga tarehe ya kuacha na iwe kwenye kumbukumbu.

*Wakati ukiiendea tarehe hiyo ya kuacha hakikisha unapunguza kiwango cha uvutaji kadiri unavyoisogea siku hiyo. Jipangie muda mrefu zaidi ya kuvuta kulingana na kiwango chako cha uvutaji na kuendelea kuuongeza kila siku ili uzoee kukaa saa nyingi bila kuvuta.

*Fuata ratiba mbadala uliyojiwekea kuziba pengo la uvutaji, kama umepanga kutumia kahawa kila unapokuwa mpweke sebuleni hakikisha unajizoeza ili ikifika tarehe yako ya kuacha usiwe mtu wa kujiuliza cha kufanya nyakati ambazo utakuwa na hamu ya sigara.

*Lengo lako liwe ni kufanikiwa na usikate tamaa utakaposhindwa kufanikisha lengo lako kwa wakati uliojipangia. Mara kwa mara nenda kamuone daktari mshauri ili akupe muongozo zaidi wa kukusaidia na ikiwezekana akupe nafasi ya kuwatembelea wagonjwa waliopata ugonjwa wa kifua kwa sababu ya kuvuta sigara.

Kwa kifupi hizo ni dondoo chache tu za kukusaidia kuachana na uvutaji wa sigara, lakini mara nyingi kinachoweka nguvu za kufanikisha uachaji wa sigara ni utashi wa mtu ambao hutokana na tathimin ya kina ya muhusika na mtazamo wake juu ya sababu za kuacha. Mara nyingi wanaoshindwa ni wale ambao hawakuzitia nguvu sababu za kuacha kwao.

Siku zote mwanadamu anaongozwa na utashi na kila mwenye kutaka hufanikiwa. Hii ina maana kuwa kama mwanadamu atasema hawezi kuacha kitu fulani, haina maana kama hawezi kwa sababu ameshindwa kujizuia bali ameamua kutokutaka na kinachomshinda ni matokeo ya  maamuzi yake. Kila anayetaka jambo hufanikiwa na hata wavutao sigara wanaweza kuacha kama wakitaka kufanya hivyo.

KUUMWA TUMBO WAKATI WA HEDHI


KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya.Kutokana na simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata akina mama wengi wakati wa hedhi nimeona ni bora niandike makala hii ili iweze kuwasaidia na wengine kujua nini chanzo na mhusika afanye nini pale anapopatwa na tatizo hilo.

Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.

Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu hayo huanza pale yai linapotoka katika mrija (fallopian tube) na kuteremka chini ya mrija huo wakati wa Ovulation.

AINA YA MAUMIVU
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.
  • Ya kwanza  ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. 
  • Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. 
  • Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.


Aina ya pili  ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.

Nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia kumi mpaka kumi na tano  wanasema kuwa hupata maumivu makali.

Uchunguzi unaonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.

Sababu hizo ni kama  kuwa na umri wa chini ya miaka 20, kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo, kutoka  damu nyingi wakati wa hedhi, wanawake ambao hawajawahi kuzaa.

Magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:

Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo.

Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaota katika mfuko wa uzazi.

PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.

  1. Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
  2. Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.
  3. baadhi ya magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. niliishia kuelezea ugonjwa wa uvimbe katika nyonga ambao husababishwa na magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya zinaa.


Dalili za ugonjwa huo ni:

  • Maumivu kuja na kuondoka, kwa kiwango tofauti (spasmodic).
  • Maumivu zaidi huwa sehemu ya chini ya tumbo na huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo ambayo husambaa mpaka mapajani.
  • Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.
  • Kupata choo laini au hata kuharisha na wengine hufunga choo.


TUMBO KUWA KUBWA AU KUWA GUMU.

  • Kupata maumivu ya kichwa, kujisikia kuchoka.
  • Kiwango cha maumivu ya tumbo la hedhi na mchanganyiko wa dalili inategemea mtu na mtu, mtu mwingine anaweza akawa anapata karibu dalili zote nilizozitaja hapo juu na mwingine ni baadhi tu au hata dalili moja. Wanawake wengi hujitambua  bila hata msaada wa daktari.


USHAURI
Iwapo mwanamke atapata maumivu makali sana ni bora akamuone daktari ili wafanye vipimo kama vile Ultrasound, CT na CT-Scan, MRI na vinginevyo ili kufahamu nini chanzo cha  maumivu hayo kuwa makali.

MATIBABU
Matibabu ya maumivu ya tumbo la hedhi kwa kawaida huweza kutibika kwa urahisi kwa kutumia vidonge vya kupunguza maumivu, kama vile Ibuprofen, naproxen au aina nyinginezo za vidonge visivyokuwa na steroids (NSAIDS). Pia kuna wakati madaktari wanaweza kumshauri mgonjwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba, Vidonge hivyo huzuia mzunguko wa yai au Ovulation na kupunguza ukali wa maumivu ya tumbo la hedhi.

Pia  wanawake wanashauriwa kufanya baadhi ya vitendo ambavyo hupunguza maumivu  hayo, kama kuoga maji moto, kuweka kitambaa chenye joto katika sehemu ya chini ya tumbo, kufanya mazoezi kama yoga, meditation,  kutumia vidonge vya vitamin E, Thiamine na Omega 3 kumetajwa kuwa husaidia katika suala hilo. Wanawake wanaopatwa na matatizo kama

hayo ni bora wapumzike vyema na kupata usingizi wa kutosha.
Vilevile unaweza kujiepusha na kupatwa na maumivu ya tumbo la mwezi kwa kufanya yafuatayo:
Kujitahidi kula matunda, mbogamboga na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi, pombe, kafeini, sodium na sukari, kufanya mazoezi ya viungo, kujiepusha na wasiwasi na mawazo na kuepuka kuvuta sigara.

Jinsi mgonjwa wa kisukari anavyoweza kuepuka kiharusi (kupooza) au stroke


Ni dhahiri kuwa wagonjwa wengi siku hizi wamekuwa wakikumbwa na tatizo hili la kupooza ambalo wengi huwakumba ghafla wakiwa hawana ufahamu wowote nini ambacho kimetokea.

KUPOOZA
Hii ni ile hali ya kiungo kupoteza utendaji kazi wake kwa sababu ya neva za fahamu kuathiriwa.

2.       KIHARUSI AU STROKE
Hii ni ile hali ya ubongo kupata hitilafu katika kupokea damu na hatimaye kupelekea kupooza kwa viungo baadhi au mwili mzima. Na endapo seli za ubongo zikikosa damu na oksijeni kwa dakika 3 zinaanza kufa na kupoteza utendaji kazi wake na endapo hili tatizo lispo shughurikiwa ndani ya masaa matatu dalili zake zinakuwa zimefikia pabaya sana katika matibabu.

Sasa basi ningependa kuongelea kidogo kuhusu ugonjwa huu na jinsi gani unaweza kujizuia.


SABABU ZISIZO EPUKIKA
Napenda kusema kwamba, Katika kitabu cha The China Study kilicho andikwa na Prof. Collin Campbell kinasema kwamba, kila binadamu ana chembe chembe za vina saba yani DNA za urithi kutoka kwa wazazi wetu ambazo zinarithishwa kila kizazi. Hivyo kila mtu ana viini vya urithi vya magonjwa mbalimbali kutoka kwa wazazi wetu, ni jukumu lako kufanya chembe chembe hizo zijioneshe wazi wazi. Hivyo bwana Campbell ambaye ni mtafiti mashuhuri wa lishe na magonjwa alisema kuwa, ni jukumu lako wewe kuuchokoza mwili wako uwezo kuonesha magonjwa ambayo umeyarithi kutoka katika ukoo wenu. Endapo ukiishi maisha ya kiafya, kula vizuri vyakula vya asili hutasumbuka na magonjwa tabia kama kisukari,shinikizo la damu,uvimbe kwenye kizazi,ugumba,kansa nk.

Kwa sababu tumeshindwa kuishi maisha ya uhalisia wetu,tunaishi kwa kufurahia vyakula vilivyofanyiwa marekebisho na binadamu na kufurahia bei yake ilivyo ndogo katika kiwango cha kujitosheleza, Basi swali la kujiuliza ni kwa nini vyakula hivyo vya viwandani vinauzwa bei ya chini sana kuzidi vyakula asili? Hebu nenda leo ukanunue nyanya ambazo unaweza kukamua ukapata chupa moja ya 400mls! UTAGHARIMIKA PESA KUBWA KULIKO YULE ALIYENUNUA Nyanya iliyotengenezwa kiwandani na kuwekwa kwenye chupa maalumu, Jiulize tena Kwa nini vinauzwa bei ya kiwango cha chini kiasi hicho?

Mwenendo huo wa maisha ya ulaji vyakula vya viwandani,vinywaji vyenye sukari nyingi,radha,rang ink, unatufanya tuwe na vihatarishi vya kupata ugonjwa wa kupoooza bila kuwa na uwezo wa kuepuka hadi pale tutakapo badili mwenendo wa maisha yetu.



1.       UMRI
Tafiti zinaonesha kuwa kadri umri wako unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo unavyozidi kuwa hatarini sana kukumbwa na tatizo la kupooza. Umri Zaidi ya miaka 50 upo katika hatari kubwa sana ya kupata magonjwa yatakayokupelekea kupata kiharusi. Kwani kiharusi ni ugonjwa moja wapo utakao kupelekea kupooza kwa baadhi ya viungo vya mwili wako na haimaye mwili mzima.
Hivyo kama wewe bado hujafikia katika umri huu, basi ni wakati wa kuishi katika lishe asili  Inatoka katika mashamba yetu ya wakulima.


2.       JINSIA
Tafito zinaonesha kwamba wanaume wako hatarini sana kupata kiharusi ukilinganisha na jinsia ya kike. Lakini pia tafiti zinaonesha kuwa kati ya mwanamke na mwanaume, mwanamke ndiye yupo hatarini sana kupata kifo kitokanacho na kiharusi. Hivyo endapo mwanamke akipatwa na kiharusi maendeleo yake kuanzia anapopatwa na tatizo huwa sio mazuri sana ukilinganisha na mwanaume. Hivyo mwanamke huwahi kukutwa na kifo Zaidi ukilinganisha na mwanaume anaweza kukaa muda mrefu sana.

3.       URITHI
Kuna watu wenye historia kuwa katika ukoo wao kuna watu wenye matatizo ya kiharusi au babu, bibi alikumbwa na tatizo hilo. Hivyo hata wewe unaweza ukawa hatarini kupata tatizo kama hilo endapo tu maisha unayo ishi nayo yakiwa ni maisha yasiyo jumuisha lishe ya asili ninayopenda kuita lishe ya dawa.

4.       KAMA UMESHAWAHI KUPATWA KIHARUSI KIDOGO
Hii ni aina ya kiharusi inayotokea kwa muda mfupi na kupotea. Muda mwingine huwa ni vigumu kutofautisha na kiharusi chenyewe. Maana kiharusi kidogo (Transient Ischemic Attach) husababisha pia viungo kupoteza utendaji kazi wake na inaweza pia kuathiri utendaji kazi wa ubongo kiakiri pia. Hivyo kama umeshaga wahi patwa na TIA kipindi cha nyuma, uwezekano wa kupata tena ni mkubwa sana, na unaweza kupata kiharusi kabisa chenyewe.


Hapo juu nimesema kuwa ni vihatarishi visivyozuilika LAKINI ni kwa wale wasioweza kubadili mienendo ya maisha ya kifahari na kujiepusha na magonjwa tabia kama kisukari,shinikizo la damu na kiwango kikubwa cha lehemu mwilini mwako


SABABU UNAZOWEZO KUZISABABISHA WEWE MWENYEWE NA KUKUPELEKEA KUPATA KIHARUSI ( STROKE)

1.       MAGONJWA YA MOYO
Magonjwa ya moyo kwa umri Zaidi ya miaka 60 imekuwa ni kawaida kutokana na miili yetu kuwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini mwetu na miili yetu kuwepo katika mazingira ya kupokea vyakula visivyo vya msingi katika kuboresha utendaji kazi wa mwili wako na tofauti na kuharibu uwezo wa mwili wako kufanya kazi ipasavyo.

Moja wapo ya magonjwa yanayopelekea kupata kiharusi, ni pale moyo wako unaposhindwa kutengeneza umeme wa kutosha kutoka juu kwenye vyumba vya moyo viitwavyo Atria na hatimaye kusambaa kwenye vyumba vya chini vya moyo viitwavyo Ventriko. Hivyo basi napenda kukuambia kuwa, moyo hutengeneza umeme, na umeme huo huzunguka kwenye sakiti ya umeme wa moyo, sakiti hio huanzia kwenye vyumba vya juu vya moyo na kushuka vyumba vya chini na hatimaye kusambaa katika misuli yote ya moyo na hatimaye kusukuma damu kutoka kwenye moyo. Hivyo kunapokuwa kuna hitirafu katika utengenezwaji wa umeme kuanzia sehemu husika, umeme unatengenezwa usiotosheleza na unatoka sehemu mbalimbali (sio maalumu) unajikuta misuli ya moyo inapata umeme kutoka katika vyanzo tofauti na umeme huo hautoshelezi kuweza kusukuma damu ipasavyo. Ugonjwa huu kwa lugha ya kiratini tunaita Atrial Fibrillation. Hivyo moyo wako unapokuwa na tatizo hili, hata mapigo ya moyo hubadirika. Njia pekee ambayo unaweza ukajigundua kuwa una tatizo hili, ni kuangalia kiashiria cha mapigo ya moyo sehemu mbali mbali kama shingoni,juu ya mkoni wako karibu na kiganja kama mapigo ya moyo yanaenda sawa au laa! Pia unaweza kwenda Zaidi kufanya uchunguzi kama kipimo cha ELECTROCARDIOGRAM (ECG) unaweza kupata majibu halisi kuwa umeme huo unajitosheleza au laa! Na unatengenezwa kutoka katika chanzo kimoja au laa! Pia moja ya sababu moja wapo ni kuangalia misuli ya moyo na kiwango cha damu kinachosukumwa na myo wako, ni vyema pia ukipata kipimo kingine cha moyo kinaitwa ECHOCARDIOGRAM(ECHO) hiki kinakupa taarifa zote za kiwango cha damu kinachosukumwa,ukubwa wa misuli ya moyo, na taarifa zinginezo. Kumbuka vipimo hivi vinapatikana katika hospitali kubwa za rufaa na vinategemea umahili wa mpimaji na msomaji wa majibu yako.

Ugonjwa huu wa moyo unaweza kusababisha kiharusi kwa sababu moja kuu kwamba, pale moyo unaposhindwa kutenegeneza umeme wa kutosha kusukuma damu, kutakuwa na mrundikano wa tamu kwenye moyo na damu hio inaweza kuganda na hatimaye kusukumwa kwenda kwenye mishipa midogo ya ubongo na kusababisha kizuizi cha damu kufika kwenye ubongo kwa sababu ya kutwama kwa damu iliyo ganda. Hivyo ndivyo unaweza kupata kiharusi endapo moyo wako hautengenezi vizuri umeme wake.





2.       KIWANGO KINGI CHA CHOLESTERO(LEHEMU) MBAYA MWILINI MWAKO

Lehemu kwa tafsiri nyepesi ni fati(mafuta) ambayo ipo kama nta ( wax) huzunguka sehmu mbalimbali katika mwili wako kwa kupitia mfumo wa mzunguko wa damu.
Ikumbukwe Lehemu ina kazi kubwa sana miilini mwetu kama kutengeneza seli za mwili na kutengeneza homoni za miili yetu na kazi zingine nyingi. Hivyo basi ningependa kukuambia kuwa kuna ina kuu tatu za lehemu ambazo ningependa kuzitaja kwa ufupi katika makundi makuu mawili, Lehemu mbaya ambayo inajulikana kama Low density Lipoprotein (LDL)  pia na Triglycerides na aina ya pili ni lehemu nzuri ijuilikanayo kama Hingh density Lipoprotein –HDL.

Lehemu inaweza kusababisha kiharusi kwa sababu ya tabia yake mbaya ya kunasa kiurahisi kwenye kuta za mishipa ya ateri na hatimaye kupunguza kipenyo cha mshipa wa damu au kuziba kabisa na hatimaye kuzuia damu kufika vizuri katika ubongo na hatimaye ubongo hukosa damu na oxygen.

Tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa nyama za aina yoyote ile, zina kiwango kingi sana cha lehemu mbaya ambayo inaenda kutuathiri sana. Lakini pia tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa vyakula vya mboga za majani, matunda vinasaidia sana kuepukana na lehemu mbaya na kumaliza kabisa matatizo yanayo sababishwa na lehemu mbaya mwilini mwako.
Rehemu hujulikana kama kisababishi kikubwa cha aina moja wapo ya kiharusi kinachosababishwa na mishipa midogo ya damu kutopitisha damu na kuulisha ubongo wako vizuri na hatimaye seli za ubongo huanza kufa nah ii hutokea baada tu ya ubongo kukosa damu kwa muda wa dakika tatu.

Aina hii ya kiharusi huitwa ISCHEMIC STROKE (Ischemia, Ni ile hali cha seli za mwili kufa Kwa kukosa oxygen, na Stroke ni kupooza). Hivyo Ischemic stroke ni kupooza kunako sababishwa na kukosa hewa ya oksijeni kwenye ubongo kwa sababu ya kukosa damu kwenye ubongo kunakosababishwa na kuziba kwa mishipa midogo midogo inayopeleka damu kwenye ubongo.

Unaweza kuchunguza kiwango chako cha lehemu kama kingi au laa! Unaweza kwa kuchunguza kitalamu kwa kuchukua sampuli ya damu na kupeleka maabala (Biochemistry Lab) na hatimaye utapata majibu yako. Pia unaweza ukatumia vipimo vingine vya picha vinavyopima kiwango cha lehemu mbaya moja kwa moja kwenye mishipa ya damu Angiogram na pia unaweza kupima kwa kutumia Kipimo cha kuangalia uzalishaji wa umeme kwenye moyo kwani lehemu ni chanzo kikubwa sana cha kuharibu utendaji kazi wa moyo hivyo kipimo cha Electrocardiogram kinaweza pia kutumika na kuangalia moja kwa moja.



Note: Napenda kutoa angalizo kuwa vipimo vingi ninavyotaja hapo ni vikubwa sana na gharama yake kidogo kubwa na vingi vinapatikana hospitali ya rufaa na kwenye vituo mbali mbali binafsi. Na hivyo wengi wenu mmekuwa mkiniuliza kama Dr Boaz Mkumbo naweza kuwasaidia kwa hilo. Napenda kuwasaidia kama ninavyokupatia elimu hii ya afya bure kabisa, ushauri wangu ni kwamba vipimo vyote vya kitaalamu vinategemea na mpimaji na msomaji ana taaluma gani katika kusoma majibu.

Kama mpimaji akipotosha na daktari anayetibu atapotoka na hapa ndipo madhaifu makubwa ya vipimo hivi vingi na ndio maana magonjwa mengi tunashindwa kuyabaini mapema kwa kukosekana kwa ufanisi kwa watu wanaopima. Sasa ningependa kukupa siri moja ya vipimo vyote nilivyo vitaja hapo juu, Vina hitaji umahili mkubwa wa kusoma majibu, na vituo vingi binafsi havina watu mahili wa kusoma vipimo hivi ,viko pale kama kitega uchumi kukushusha roho kuwa umepima. Tatizo sio kupima, Kiu ni kugundua ugonjwa sahihi na utibiwe upone. Ningependa kukushauiri kama unahitaji vipimo hivi, fika hospitali yenye wataalamu wa kutosha wenye uwezo mkubwa wa kukupa majibu ya uhakika ya kukata kiu yako.

- American Diabetes Association Inashauri kiwango cha LDL cholesterol kuwa chini ya 100 mg/dl kwa watu wenye kisukari na chini ya 70 mg/dl kwa watu wenye magonjwa ya moyo.
-Pia inashauri kuwa kiwango cha lehemu nzuri yani HDL iwe 50 mg/dl au Zaidi kwa wanawake na kwa wanaume HDL iwe 40 mg/dl au Zaidi.


3.       SHINIKIZOLA JUU LA DAMU( HIGH BLOOD PRESSURE)
Shinikizo la damu ni msukumo wa damu ndani ya mishipa ya damu thidi ya ukuta wa mishipa. Shinikizo la damu lenye takwimu ya Zaidi 140/90 mmhg kwa muda mrefu utakuwa unastahili kuitwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu.

Shinikizo kubwa la damu husababisha kiharusi kwa kusababisha mishipa midogo ya damu ya ubongo kupasuka na hatimaye damu kuvia kwenye ubongo. Aina hii ya kiharusi huitwa Hemorrhegic Stroke. Aina hii ya kiharusi ni mara chache sana kutokea na huwa ni nadra sana kukuta mtu ana aina hii ya kiharusi lakini ndio aina nambari moja inayoweza kusababisha kifo haraka sana kwa mgonjwa. Kwani wagonjwa wengi wanaopata aina hii ya kiharusi huwa maendeleo yao sio mazuri na wengi hufika hospitali wakiwa hawajitambui kabisa.

Ugonjwa wa Shinikizo la damu unazuilika kabisa kwa kufuata masharti machache kama haya hapa chini:
Ulaji wa vyakula vya madini ya potasiamu hadi kufikia 3900mg kwa siku kutoka kwenye ndizi,machungwa,matunda yaliyo kaushwa,viazi vitamu nk

Ulaji wa Madini ya Calcium angalau 1200mg kila siku kutoka kwenye vyakula kama mtindi na maziwa ya kuwaida

Ulaji wa vyakula vyenye magnesium angalau 420mg kwa siku kwa wanaume na 320mg kwa wanawake kutoka kwenye vyakula kama Spinachi, nafaka isiyokobolewa, Ndizi nk

4.       KUTOFANYA MAZOEZI YA VIUNGO
Mazoezi siku hizi yamekuwa yakitumiwa na watu pekee wanao hitaji kupunguza mwili na kupunguza nyama uzembe ( belly fats) ,inapendeza sana wadada wengi kuchukia kubadirika kwa miili yao unaotokana na ulaji wa vyakula visivyo asili, Napenda kukuambia kuwa Mazoezi pekee sio SULUHISHO LA KUPUNGUZA MWILI WAKO, NA WALA SIO SULUHISHO LA KUONDOA NYAMA UZEMBE. Bali siku ukijifunza kubadili mwonekano wa sahani yako mezani utafurahia jinsi uzito unavyopungua! Najua huamini, lakini unapokuwa unaanza safari ya kupunguza uzito na nyama uzembe ujue ni safari nzito kama vile safari ya kutafuta pesa. Kupungua uzito sio kurahisi ingekuwa rahisi wengi hawapendi wangekuwa wameshapungua ! Njia pekee ni kujidhatiti na kudhubutu pekee katika kubadili lishe yako, mchawi mkubwa ni sahani yako unayoiweka mbele yako kila utakapo kuweka kitu kinywani mwako.

Mazoezi huimarisha viungo na mzunguko wa damu na kusaidia mwili wako kutoa taka ambazo zimepatikana kutokana na shughuli za mwili.

Tafiti zinaonesha kwamba watu ambao hawafanyi mazoezi ya kutosha katika umri mkubwa huwa hatarini kupata kiharusi aina ya Ishemic stroke inayosababishwa na damu kutosukumwa ipasavyo katika mishipa ya damu na kusababisha  emboli kunasa kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kufika vizuri katika ubongo.


MAKUNDI MENGINEYO AMBAYO SITAPENDA KUYAELEZA KWA KINA LEO
5.       Walevi wa pombe na sigara

6.       Wanaotumia njia za uzazi wa mpango kwa muda mrefu

7.       Watu wenye kisukari kwani kisukari na shinikizo la damu ni bwana harusi na bibi harusi mara nyingi hutembea kwa umoja.


90 DAYS CARDIO FUNCTION-REVERSE PACKAGE
Hii ni program maalumu kwa wasomaji wetu ambao wamekuwa wakisumbuka na magonjwa sugu kama kisukari,shinikizo la juu la damu n ahata shinikizo la chini la damu, kiharusi n ahata tatizo la kupungua kwa utendaji kazi wa ubongo.

Hii program imeandaliwa na Boaz Mkumbo ambapo inawafaa wale wachache wanaohitaji msaada wangu pale walipofikia kutumia elimu hii ya afya ambayo nimekuwa nikiitoa kila siku.

                                  NDANI YA CARDIO FUNCTION REVERSE PACKAGE
1.       Unajipatia msaada wa kupata Suluhisho la kuondoa lehemu zote mbaya mwilini mwako na kuimarisha mzunguko wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili na kuimarisha damu inayoenda kulisha ubongo.

2.       Utajipatia Kiondoa sumu makini kabisa chenye kuzuia mchakato unaendelea mwilini mwako ( Gut and systemic Inflammation) chenye kusheheni madini mengi ambayo ni catalyst ya shughuri nyingi za mwili madini haya husaidia kuupooza mwili kutoka katika mpambano wa maradhi mbali mbali yanayoendelea mwlini mwako, Madini mengi ya Manganeze,zinc,selenium,Iron na mengine mengi kwani kimekuwa ni chakula nambari tatu kama lishe bora duniani

3.       Unaweza kupatiwa ushauri kwa wale waliotayari pata tatizo la kupooza kutokana na kiharusi na presha yako haijakaa sawa, Utapewa huduma nzuri namna gani unaweza pia ukanufaika na mazoezi ya viungo na bidhaa zetu unapokuwa katika matibabu chini ya ushauri wetu.

4.       Napenda kuwaambia kuwa msaada huu ndani ya package hii ya siku 90 tutakusaidia endapo tu , unahitaji kwani wengi wanafurahia huduma zetu za tiba asili na pia ushauri tunatoa kwa watu wenye matatizo ya magonjwa haya sugu.

Saturday, April 16, 2016

Makamu Wa Rais Mama Samia Suluhu Amfuta Machozi Millen Magese Mapambano Dhidi Ya Endometriosis ( Kuziba Mirija ya Uzazi )


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu amemfuta machozi Mwanadada, Happiness Millen Magese ambaye ni shujaa wa kipekee kutoka Afrika dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa Endometriosis.

Mama Samia amechukua hatua hiyo jioni ya 15 Aprili 2016 wakati wa hafla maalum ya kumkabidhi tuzo.

Katika kilio chake hicho, Millen kimemfanya Mama Samia kumfuta machozi na kumpa kitambaa, mwanamitindo huyo huku akimweleza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana naye kwani tatizo hilo si la Millen pekee bali ni kwa wanawake wengi hapa Tanzania.

Mama Samia alimwambia kuwa, tatizo alilonalo la kuziba kwa mirija ya uzazi litapata ufumbuzi na kutaka asilie kwani Serikali inania njema kwa watu wake hivyo wataendeleza juhudi Zaidi huku akifungua milango na mwanadada huyo.

Suluhu alisema kuwa hata yeye tatizo kama hilo lipo katika familia yake, lakini ana amini kwa ushirikiano wa mwanamitindo huyo tatizo hilo linapewa uzito. 
Alisema kuwa ni kitu kilichokuwa kikimuumiza sana kichwa, ana amini kupitia Millen hata binti yake atapata nafuu.

"Nimefurahi kukutana nawe na Serikali haitakuangusha tutakuunga mkono katika kuhakikisha gonjwa hili linapata ufumbuzi na kutoa elimu kwa kila mtanzania kulitambua"alisema.

Akizungumza kwa upande wake Magese alisema amekuwa akifanya semina mbalimbali kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, kuwaelimisha wanawake kuhusu endometriosis.

Alisema Machi 30, mwaka huu Taasisi ya Millen Magese ilikusanya vijana (hususani wa kike) wapatao mia tano kutoka shule za Mugabe, Manzese, Salma Kikwete na Turiani, kuwafundisha, kuwatahadharisha na kuwatanabahi kuhusu Afya, Uenendo, Maisha yao ya kila siku na Changamoto zilizo mbele yao na hususani ikilenga zaidi watoto wa kike ambao wao ndio wahanga wa ugonjwa wa Endometriosis.

Magese alisema watoto hao wakiwafikia hata wenzao 20 tu kila mmoja basi takribani watu elfu kumi watakuwa wamefikiwa.

Alisema ni mwanzo tu angependa kupata ushirikiano na msaada wa Serikali ili afike kila pembe ya nchi yetu hii na kufikia wengi iwezekanavyo.

"Ninaamini -Nikiokoa hata nafsi moja kuna wakati ambao inatosha kwani nafsi hiyo yaweza kuokoa walio wengi zaidi,shabaha yake ni kuona wanawake wenye ugonjwa huo wanapata tiba mapema ili waweze kubaki na uwezo wao wa kushika mimba na kuzaa kwa njia ya kawaida" alisema Magese.

" Mimi nilichelewa na nimejikuta nikipoteza uwezo wa kushika mimba, kwa hiyo siwezi tena kupata mtoto kwa njia ya kawaida, Kibaiolojia.

"Nimeshafanyiwa oparesheni mara 13 kati ya Afrika Kusini na Marekani. Na sasa mirija yangu yote ya uzazi imeziba, vilevile upande mmoja wa ovari haufanyi kazi.

"Naahidi kupambana na ugonjwa huu mpaka mwisho. Pamoja na jitihada zote, lengo langu la juu ni kuhakikisha napata uwezo wa kujenga hospitali kubwa kupitia taasisi yangu ya Millen Magese (Millen Magese Foundation) ambayo itajishughulisha zaidi na utoaji wa tiba ya endometriosis kwa wanawake. Namuomba sana Mungu anisaidie." Alisema Millen

Alisema lengo lake kuu na Taasisi yangu ni kujenga hospitali maalum ya magonjwa ya wanawake hapa nchini.

"Nitashukuru sana iwapo Serikali yako tukufu itatusaidia kupata eneo la kutosha na kutupa muongozo na uwezeshaji mwingine utakaohitajika kadri harakati zitakapokuwa zikiendelea".

Alisema tayari Taasisi ya Millen Magese kwa kushirikiana na ProjectCure ya Marekani imeweza kukusanya vifaa vinavyohusu afya ya mwanamke vyenye thamani ya takribani dola laki moja , ningeomba sana Serikali yako Tukufu kutusaidia kuweza kusafirisha na kuviingiza vifaa hivyo nchini (kwa maana ya taratibu, gharama za usafirishaji na kodi husika).

"Kwa namna moja ama nyingi napenda kuishukuru Wizara ya Afya kupitia kwa Waziri wake Ummy Mwalim na Naibu Waziri Hamis Kingwangwalah, pamoja na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, kwa uhirikiano wao na taasisi yangu ya Millen Magese, katika kuhakikisha tunafanikisha suala la ujenzi wa kituo cha Hospitali.

"Tuko katika maengezi na Hospitali ya Kairuki, ambao wamejitolea kuungana name katika ksaidia tatizo hili, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Hospitali za Serikali katika kusaidia wanawake wenye tatizo hilo.

"Hospitali ya Kairuki imejitolea kusaidia wanawake wenye matatizo hayo, nina amini kwa ushirikiano wake Mhe. Makamu wa Rais, tatizo hili litapewa uzito unaostahili.

"Mheshimiwa Makamu wa Rais,Elimu ya masuala ya uzazi na afya ya mwanamke zifundishwe kwa wadogo zetu, tusichelewe na baadhi yao yakawafika madhla haya yasiyomithilika kama yangu, wakati mwingine huwa nahisi kama visu vinapit tumboni mwangu, natapika, nazimia, nashindwa hata kufanya kazi zangu, ni hivi karibuni tu katika onesho kubwa la mavazi, nilizimia niliporudi nyuma ya jukwaa (Namshukuru Mungu kwa YOTE)

"Naendelea pia na kujitoa katika shughuli za kijamii, kama ambavyo nimeshafanya kama kujenga madarasa na uchangiaji wa madawati, kama ambavyo nimewahi kufanya mkoani Mtwara.

"Nataka pia niwe balozi mzuri wa elimu yetu.

"Mheshimiwa Makamu wa Rais, Sitaki kulia, nimeamua kuwa SAUTI. Sitaki kumuuliza Mungu kwa nini, nimeamua kupokea na kutimiza mapenzi yake. Mheshimiwa Makamu wa Rais, #UpasuajiMara13Umetosha

#TunahitajiUtafitiZaidiKupataTIBA. Daima najivunia nyumbani na popote nilipo duniani ..Tanzania imebaki kuwa tunu ya uwepo na maisha yangu.

"Mwisho nakushukuru mheshimiwa makamu wa rais kwa mkutano huu, nawashukuru wote tuliokutana hapa. Mungu AWABARIKI.

"Naomba unipe ruhusa kama ishara kukukabidhi Tuzo na Tunu mbalimbali nilizozitaja kwa Heshima ya Taifa, Nchi yangu ya Tanzania, Serikali yangu na ndugu zangu Watanzania

#NawapendaSANA.

"Kule kwetu Usukumani kwa heshima huwa tunapiga goti kama Heshima, Mheshimi wa Makamu wa Rais, Mama, nasema Wabeja SANA."

Tuesday, February 2, 2016

JINSI YA KUPUNGUZA UZITO NA UNENE KWA KUTUMIA TIBA ASILIA, TAFADHALI TEMBELEA:




7.   Matatizo  Katika  mfumo  wa  Ubongo
Uume  hauwezi  kusimama   bila  ya  kuwa  na  ushirikiano  na  ubongo.  Ili mtu  uume  uweze  kusimama, mtu  lazima  apate  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa  (UBONGO  UNA HUSIKA  HAPO ), akishapata  wazo, ubungo  hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo hupeleka  taarifa  kwenye  mishipa  ya  uume  then  uume  usimama.   
 
Hivyo  basi  ili  mtu  aweze  kuwa  na uwezo  wa kusimamisha  uume  wake  ni lazima  kuwa  na  mawasiliano  mazuri  na  imara  kati  ya mishipa  ya  fahamu ( ubongo ), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo   na  mishipa  ya  kwenye    uume.  Bila  ushirikiano  kati  ya  vitu  hivyo  vitatu, uume  hauwezi  kusimama.

Magonjwa  yanayoweza  kuathiri  ushirikiano  kati  ya  mishipa  ya  ubongo  na  mishipa  ya  uume, yanaweza  kusababisha  kushindwa  kusimama  kwa  uume.

Magonjwa  hayo  ni  pamoja  na  kiharusi,kupoteza  kumbukumbu  (  Alzheimer ), multiple  sclerosis pamoja  na  ugonjwa  wa  Parkinson.

Ni  vyema  mgonjwa  akatibiwa  kwanza  magonjwa  hayo  kabla  ya  kuanza  kutumia  dawa  ya  nguvu  za  kiume.  Kufahamu  jinsi  ya  kujitibu  magonjwa  tajwa  hapo  juu  kwa  njia  asilia,tafadhali  tembelea

Mambo   mengine  yanayo  sababisha  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  pamoja  na  maumivu & majeraha  kwenye  uti  wa  mgongo,  chango  la  kiume , ngiri  na  matatizo  katika  homoni.

VIASHRIA  VYA  MTU  MWENYE  TATIZO  LA  UKOSEFU/UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Mtu  mwenye  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  huwa  na  dalili  zifuatazo ;

1. Kushindwa  kabisa  kusimamisha  uume  wake
2. Uume  kusimama  ukiwa  legelege
3. Kuwahi  kumaliza  tendo  la  ndoa
4. Mwanaume  kutokuwa  na uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  katika  baadhi  ya  staili  ( Mara  nyingi   mwanaume  huyu huwa  na  uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa    staili  moja  tu ).  
 
Hapa  mwanaume  anakuwa  na  uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  staili  ya   “ missionary” pekee.  Ikibadilishwa   staili, mwanaume  anakuwa hana  tena  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wake  japo  katika  hali  ya lege  lege

5. Uume  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimama  wenyewe   bila  kushikwashikwa  ama  kutomaswa kwa  muda  mrefu.

6. Uume  kusinyaa  ukiwa  ndani  ya  mwanamke.

7. Uume  kusinyaa, pindi  inapotokea  activity  yoyote  ya  kiungo  ama  ogani  nyingine  ya  mwanaume  wakati  wa  tendo  la  ndoa. Kwa  mfano, wakati  wa  tendo  la  ndoa, ikitokea  mwanaume  amekohoa  au  kupiga  chafya, uume  nao  unasinyaa.

8. Uume  kusinyaa  mara  tu  baada  ya kutolewa  ndani  ya  uke ( Kwa  mfano  kama  unafanya  tendo  la  ndoa, halafu  uume  ukatoka  nje, kitendo  cha  kuushika  kuurudisha ndani, tayari  una  sinyaa )

9. Kutokuwa  na  uwezo  wa  kurudia  tendo  la  ndoa.
10.  Kupatwa  na  maumivu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

VIASHIRIA  VYA  MWANAUME  ASIYE 
NA  TATIZO  LA UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume  asiye  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, huonyesha  ishara  zifuatazo ;

i. Uume  husimama  ukiwa  imara  kama  msumari.

ii.Hukaa  kifuani  kwa  muda  mrefu  ( Wastani  ni  kati  ya  dakika  20  hadi  45  )

iii.Huweza  kurudia  tendo  la  ndoa  zaidi  ya  mara  tatu  bila  misuli  ya  uume  kuchoka.

iv. Huweza  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  staili  yoyote  ile

v. Uume  husimama  wenyewe  bila  kushikwa  shikwa  wala  kuwa  stimulated  kwa  namna  yoyote  ile

vi.Kwa  ufupi  anakuwa  na  uwezo  wa  kufanya na  kukamilisha  tendo  la  ndoa  kwa  uukamilifu  mkubwa.

TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA  UKOSEFU/UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Dawa  asilia  ya  JIKO   ni  dawa  asilia  inayo  tibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.

MFUMO   WA  DAWA
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO ni  mkusanyiko  wa  dawa  nne  asilia  zenye  uwezo  mkubwa  sana  katika kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Dawa  hizi  zipo  katika  mfumo  wa  MIZIZI  na  UNGA  UNGA.

JINSI   DOZI  YA  DAWA  YA  JIKO  INAVYO  FANYA  KAZI.
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO  inafanya  kazi  zifuatazo  katika  mwili  wa  mwanadamu.

KAZI  INAYO  FANYWA  NA  DAWA  YA  JIKO .
Dawa  ya  JIKO  inasadia  katika  mambo  makuu yafuatayo:

1.  Inasaidia   kuimarisha  mishipa  ya  uume  ulio legea  na  hivyo  kuufanya  uume  uwe  na uwezo  wa  kusimama  barabara  kama  msumari  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

2. Inasaidia  kusafisha  mishipa  ya  kwenye  uume  na  hivyo  kusaidia  katika  kuongeza  kasi  ya  msukumo  wa  damu  kwenye  mishipa  ya  kwenye  uume.

3. Huongeza  damu  mwilini

4. Husaidia  kuongeza  msukumo (pressure)  wa  damu  kwenye  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  kuwa  na  nguvu  za  ajabu.

5. Huipa  misuli  ya  uume  uwezo  wa  kuziba  wa  kuizuia  mishipa  ya  vena   kunyonya  damu  kwenye  mishipa  ya  uume  wakati  wa  tendo  la  ndoa  na  matokeo  yake  kukupa  uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  muda  mrefu( Kuzuia  hali  ya  kufika  kileleni  haraka  )

6. Husaidia  kurelax  mind  na  hivyo  kumfanya  mtu  awe  na  uwezo  wa  kuconcentrate  wakati  wa  tendo la  ndoa   bila  kuathiriwa  na  msongo  wa  mawazo

7.  Hurejesha, kuimarisha  na  kuboresha  ushirikiano  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  ya  kwenye  ubongo  (nerves), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  mishipa  ya  kwenye  uume

8. Humfanya  mwanaume  awe  na  uwezo  wa  kurudia  tendo  la  ndoa  mara  nyingi  zaidi  bila  kuchoka.
9. Husaidia  kuongeza  hamu  ya  tendo  la  ndoa.

10.Husaidia  kuurudisha  nje  uume  ulio ingia  ndani.

11. Husaidia  kutibu  side effects  za  punyeto  na  matumizi  ya  muda  mrefu  ya dawa  kali  za  (za  kizungu ) za  kuongeza  nguvu  za  kiume.

12. Husaidia  kutibu  chango  la  kiume.
13. Dawa  hii  huwasaidia  hata  wanawake  wanao sumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  hamu ya  tendo  la  ndoa.

BEI  YA  DAWA:  Dozi  ya  dawa  ya  JIKO  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU  (Tshs.80,000/=)

DAWA  HII  IMETHIBITISHWA  NA  MKEMIA  MKUU  WA  SERIKALI.

MAHALI  TUNAPOPATIKANA :
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO, inatolewa  na  duka  la  dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST    NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC. Tunapatikana  jijini  DAR ES  SALAAM, katika  eneo  la UBUNGO    karibu  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu, tunatoa  huduma  ya kuwapelekea  dawa  mahali  walipo  ( DELIVERY )

Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  DAR  ES  SALAAM, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  mabasi, wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa   njia  ya  boti  na  kwa  wateja  waliopo  Ulaya, America  na  Arabuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  DHL  au POSTA.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA
0766  53  83  84.
Na  kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, endelea  kutembelea:

www.neemaherbalist.blogspot.com

MAMBO YANAYO SABABISHA UKOSEFU/UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.



Tumeshajua   nguvu za  kiume  ni  nini, jinsi  uume  unavyo  simama, hatua  za  kusimama  kwa  uume, pamoja  na  mambo  yanayo  fanya  uume  uweze  kusimama  na  kuwa  na  uwezo  wa  kuendelea  kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Ni  vyema  tukajua  mambo  yanayo  sababisha  kushindwa  kusimama  kwa  uume, mambo  yanayo  sababisha  uume  ushindwe kuendelea  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa   pamoja  na  mambo  yanayo  fanya  mtu  ashindwe  kurudia  tendo  la  ndoa.

Yafuatayo  ni  mambo  yanayo  sababisha  ukosefu wa  nguvu  za  kiume.

1. MAGONJWA  YANAYO  SHAMBULIA  MFUMO  WA  DAMU  PAMOJA  NA  MISHIPA  YA  DAMU.

Damu  ndio  nishati  inayo wezesha  kusimama  kwa  uume  na kuufanya  kuwa  mgumu na  imara  kama  msumari.

Damu  ndio  nishati  inayo weza   kuufanya  uume uendelee kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Damu  ndio  nishati  inayo  upa  uume  uimara  na  uwezo  wa  kurudia  tendo  la  ndoa  zaidi  ya  mara  moja.

Hivyo  basi  ili  uume  uweze  kuwa  imara na  wenye  nguvu, pamoja  na  kuwa  na  uwezo  wa  kumudu  na  kustahimili   tendo  la  ndoa  wakati  wowote , basi  ni  lazima   mwanaume  awe  na mfumo  imara  wa  damu  utakao  ruhusu  kutiririka  kwa  damu  kwenda  katika  sehemu mbalimbali  za  mwili  ikiwamo  uume.

Ili  mfumo  uweze  kuwa  imara  ni  lazima  mhusika  awe  na  damu  ya  kutosha, na  pili  awe  na  mishipa  ya  damu  yenye  afya.

Katika  mwili  wa  mwanadamu,kuna  mishipa  inayo  tumika  kusafirisha  damu  kutoka  katika  sehemu moja  ya  mwili kwenda  katika  sehemu  nyingine  ya  mwili  ikiwemo  uume. Mishipa  hiyo  ni  kama  vile  vena (veins), atery ( ateri) na  capillary  ( kapilari )

Mishipa  hii  ya  damu  inapaswa  kuwa  imara  na  yenye  afya  njema  wakati  wote.   Mishipa  hii  ikipatwa  na  hitilifu, basi  itazuia  kusafirishwa  kwa  damu  katika  sehemu  mbalimbali za  mwili  wa  mwanadamu  na  hatimaye  kufanya  suala  la  kuwa  na  nguvu  za  kiume  kwa  mhusika  kuwa  ugumu  kwa  sababu   ya  kushindwa  kupeleka  damu  kwenye  mishipa  ya  uume.

Magonjwa  kwenye  mishipa  ya  damu  huzuia   kutirika  kwa  damu kwenye  ogani  muhimu   kama  vile  moyo, ubongo na  figo.

VIASHIRIA  VYA  MAGONJWA  KWENYE  MISHIPA  YA  DAMU.
Utajuaje  kwamba  una  magonjwa  kwenye  mishipa  yako  ya  damu ?

Ukiwa  una  matatizo  yafuatayo ya  kiafya, ni  ishara  kwamba, una  magonjwa  kwenye  mishipa  yako  ya  damu:

1.  Kolestrol ( Ama  lehemu  kwenye  damu )
Kolestrol  nyingi  kwenye  damu, huzuia  kutiririka  kwa  damu. Kolestrol  ikizidi  kwenye  damu,  hupelekea  kuziba   mishipa  ya  ateri  ambayo  kazi  yake  ni  kupeleka  damu  kwenye  uume. Matokeo  yake  ni  mhusika  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wake barabara  kwa  sababu uume  hauwezi  kusimama  bila  damu  kuingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume.  
 
Hivyo  basi pamoja  na  dawa  ya  nguvu  za  kiume, yakupasa  kutibu  kolestrol. Unaweza  kuondoa  kolestrol  kwenye  damu  kwa  kutumia  dawa  mbali  za  asili  kama  vile mdalasini,uwatu, habbat sodah  etc.  Jinsi  ya  kujitibu  kolestrol  kwa  kutumia dawa asilia  tafadhali  tembelea


2. Shinikizo  Kubwa  la  Damu
Shinikizo  Kuu la  Damu husababisha  mishipa  ya  ateri  ambayo  hutiririsha  damu  iingiayo  kwenye  uume  kuziba  na  kushindwa kutanuka  kwa  kiwango  inachotakiwa  kutanuka.

Pia  huifanya  mishipa  laini  katika  uume   kushindwa  ku-relax  na  hivyo  kushindwa  kuizuia  mishipa  ya  vena  ya  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  maeneo  mengineyo  ya  mwilini.

Matokeo  yake  kunakuwa hakuna  kiasi  cha  kutosha  cha  damu  iingiayo  kwenye  uume  na  hivyo  kufanya  uume  ushindwe  kusimama.

Vile  vile  hata  kiasi  kidogo  cha  damu  kinacho  ingia  kwenye  uume, kinashindwa  kuendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  uume  wakati uume  ukiwa  umesimama, na  matokeo yake  ni  uume  kusinyaa  ndani  ya  kipindi kifupi  sana  tangu  usimame.

Pamoja  na kutumia  dawa  ya  nguvu  za  kiume, unapaswa   pia  kutumia  dawa  asilia  kujitibu  tatizo  la  shinikizo  kuu  la  damu.

Kufahamu  jinsi  ya  kujitibu  tatizo  la  shinikizo  la  damu  kwa  njia  ya  asilia, tembelea :


3.  Ugonjwa  wa  kisukari :
Ugonjwa  wa  kisukari  ni  miongoni  mwa  vyanzo  vikuu  vya  tatizo  la  ukosefu wa  nguvu  za  kiume.  Kusimama  kwa  uume  kunategemeana  na  kutiririka  kwa  damu  mwilini. Kisukari  huathiri  mishipa  ya  damu pamoja  na  usambazaji  wa  damu  kwenye  ogani  muhimu  mwilini  kama  vile  moyo, ubongo, figo  na  uume.

Kiukweli, mwanaume  mwenye  kisukari  yupo  katika  risk  kubwa  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume,m tena  katika  kiwango  kikubwa  sana.

Unashauriwa pamoja  na kutumia  dawa  ya  nguvu  za  kiume, tumia  pamoja  na  dawa  mbalimbali  za  asili  kwa  ajili  ya  kubalance  sukari  yako mwilini. 
 
Zipo  dawa  mbalimbali  za  asili  zinazo  saidia  kubalance  kiwango  cha  sukari  mwilini. Dwa  hizo  ni  pamoja na mdalasini, unga  wa  uwatu, mbegu  za  uwatu, manjano, majani  ya  manjano,mbegu  za  katani, nakadhalika.
 
 Namna  ya  kutumia  dawa  hizo  kujitibu  tatizo  la  sukari, tafadhali  tembelea : http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/jitibu-kisukari-presha-shinikizo-la.html

4. Magonjwa  ya  figo
Tatizo  la  ugonjwa  wa  figo  huathiri  vitu vingi  ambavyo  ni  muhimu  sana  katika  kuufanya  uume  uweze  kusimama  na  kuendelea  kudumu  katika  kusimama.

Tatizo  la  figo, huathiri  homoni, huathiri kutiririka   kwa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume. Huathiri  mfumo  wa mishipa  ya  neva  pamoja  na  nishati  ya  mwili mzima.

Pamoja  na  dawa  ya  kutibu  tatizo  la  nguvu  za  kiume, unapaswa  pia, kutibu  tatizo  la  figo.
 
 Kufahamu  jinsi  ya  kujitibu  magonjwa  mbalimbali  ya  figo  kwa  kutumia  dawa  mbalimbali  asilia, tembelea : http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/jitibu-kisukari-presha-shinikizo-la.html

5.  Ugonjwa  wa  moyo
Moyo  ndio  supplier  mkubwa  wa  damu  katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili.  Ugonjwa  wa  moyo  hupunguza  uwezo  wa  moyo  kusambaza  damu  kwenye  mishipa  mbalimbali  ya  damu  na  hivyo  kuathiri  utendaji  kazi  wa  mishipa ya  damu  kama  vile  ateri  na  vena.
 
 Matokeo  yake  ni  mishipa  hiyo  kushindwa  kupeleka  damu  ya  kutosha  katika  uume  pamoja  na  kushindwa  kuifanya  mishipa  ya  uume  kurelax na  matokeo  yake,. Ukosefu  wa nguvu  za  kiume. 
 
Hivyo  basi, pamoja  na  dawa  ya  nguvu  za  kiume, unapaswa  pia   kutibu  tatizo  la  moyo. Kufahamu  jinsi  unavyo  weza  kutibu  ugonjwa  wa  moyo  kwa  dawa  asilia, tembelea :


6.  Kupwaya  kwa  mishipa  ya  vena.
Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  kwenye  uume   kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyingine  za  mwili. 
 
 Mishipa  ya  vena  iliyopo  karibu  na  uume  kazi  yake  kubwa  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  yoyote  kwenye  mishipa  ya  uume. ( KUMBUKA  KUWA  DAMU  NDIO  HUFANYA  UUMU  USIMAME, HIVYO  CHOCHOTE  KILE  KITAKACHO  FANYA  DAMU  ISIKAE  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME , KITAFANYA  UUME  USINYAE  )

Ili  uume  uendelee  kusimama  ni  lazima, mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo  wa  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  kupeleka  nje  ya  mishipa  ya  uume.

Na  ili  mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo  wa    kunyonya  damu  kutoka  kwenye   mishipa  ya  uume  ulio  simama  na  kuipeleka  kwenye  sehemu  nyingine  za  mwili,  ni  lazima  mishipa  ya  uume  iwe  imara  na  thabiti  isiyo  na  hitilafu  yoyote  ile.

Mishipa  ya  vena  ikipwaya, mwanaume  hutokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wako, na  ikitokea  umefanikiwa  kuusimamisha  basi  utasimama  ukiwa  legelege  sana  na  utasinyaa  ndani  ya  muda  mfupi  sana, kwa  sababu  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  uume  wako  na  kuufanya  usimame, itanyonywa  ndani  ya  muda  mfupi  sana  na  kutolewa  nje  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  wako  usimame.

Tatizo  la  kupwaya  kwa  mishipa  ya  vena  linasababishwa  na  kupiga  punyeto  kwa  muda  mrefu  pamoja  na  ugonjwa  wa  kisukari.

KUPIGA  PUNYETO  KWA  MUDA  MREFU:  Kupiga  punyeto  kwa  muda  mrefu  ni  moja  kati  ya  vyanzo  vikuu  vya  tatizo  la  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  Asilimia  kubwa  ya  vijana  wenye  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, linasababishwa  na  upigaji  wa  punyeto  kwa  muda  mrefu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Unapopiga  punyeto  unakuwa  unaiminya  mishipa  ya  uume   ambayo  ndio  inaufanya  uume  usimame.

Matokeo  yake  unaifanya  mishipa  hiyo  ilegee na  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimama  tena.

Mishipa  ya  uume  iliyo  legea  kutokana  na  upigaji  punyeto, huleta  madhara  yafuatayo  :

i. Huondoa  uwezo  wa  mishipa  ya  uume  kurelax.
( Unapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  uume  ina relax  , mishipa  iki  relax  husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuruhusu  damu  kingie  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hatimaye  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  mgumu)

ii.Mishipa   ya  kiume  ikishindwa  ku relax  husababisha  mishipa  ya  ateri  kuziba

iii. Mishipa  ya  ateri  ikiziba, damu  haiwezi  kutiririka  kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, na  hata  ikitokea  damu  imeingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume  basi  huingia  kiasi  kidogo sana   tena  kwa  presha  ndogo  sana  hivyo  basi  hata  kama  uume  utasimama   basi  utasimama  ukiwa  legelege  sana

iv.Mishipa  ya  uume  ikishindwa  kurelax  basi  haitakuwa  na  uwezo  wa  kuipush  na  kuiziba  mishipa  ya  vena  ambayo  ndio  hunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  ulio  simama. Matokeo  yake  basi, damu  kidogo  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuufanya  uume  kusimama, hunyonywa  na  kutolewa  nje  ya  mishipa  ya  uume  ndani  ya  sekunde  chache  sana  na  hivyo  kuufanya  uume usinyae  ndani  ya  muda  mfupi  sana.

v.         Mishipa  ya  uume  kulegea
vi.       Uume  kurudi ndani  na  kusinyaa  na  kuwa  kama  uume  wa  mtoto

6. Tatizo  la  unene  kupita  kiasi : Tatizo  la  unene  na  uzito  kupita  kiasi  ni  miongoni  mwa  mambo  yanayo  sababisha  upungufu  wa  nguvu  za  kiume. Unene  kupita  kiasi  humuweka  mtu  katika  hatari  ya  kupatwa  na  magonjwa  kama  vile  kisukari, presha, moyo  na  shinikizo  kuu  la  damu. 
 
Na  magonjwa  ya  kisukari, moyo,presha  na  shinikizo  la  damu  husababisha  upungufu na  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, na  hivyo  kumuweka  muhusika  katika  hatari  kuu  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Hivyo  basi  kwa  wewe  mwenye  tatizo  la  unene  na  uzito  kupita  kiasi , pamoja  na  kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume,  ni  vyema  ukafanya  na  mpango  wa  kupunguza  unene  na  uzito  wako.

JINSI  YA  KUPUNGUZA  UZITO  NA  UNENE  KWA  KUTUMIA  TIBA  ASILIA, TAFADHALI  TEMBELEA: